“Siwezi kufanya hivi tena. Siwezi kuwa na wewe bila kukuona kwa namna ninavyotaka mimi. Shauku ya wewe kuwa wangu inazidi maadili yangu, inazidi uwezo wangu wa matamanio. Siwezi tena kujifanya kama sioni jinsi gani nikiangalia macho yako na kujidanganya kwamba… chochote tulicho nacho… kinaenda kwa jinsi unavyotaka.” “Sijui nifanye nini ili uhisi ninavyohisi mimi. Labda huwezi kuona hili, lakini angalau jaribu kunitaka kama ninavyokutaka mimi, tumegawana hisia zetu, matatizo yetu, miili yetu. Kwanini iwe vigumu kuukubali uhalisia wa mahusiano yetu?” “Unanipenda?” Swali hilo. Swali ambalo hutaki kulisikia masikioni mwako. Swali ambalo huna jibu nalo. Kutarajia jibu kutoka kwa mtu usiyemtaka kumpoteza ni kama kisu kichanjacho moyoni. Ninajua hilo, kujua kwamba jibu litakalotoka litauma hata kama watabaki au kuondoka. Unatazama macho yake yaliyojaa hasira, ukihisi njaa iliyoko kwenye mtazamo wake. Maneno yanakukwama kooni na kushindwa kuongea. Unashusha macho, ukitamani aseme c...
Welcome to Nuru Narrative, mahali ambapo creativity na ubunifu hukutana. This blog is a celebration of stories, adventures, and reflections told through a unique blend of Kiswahili na English, connecting cultures and bridging ideas across languages. Kwenye Nuru Narrative, utapata mchanganyiko wa hadithi fupi za kuvutia, heartfelt travel journals, na tafakari kuhusu maisha. Each story is carefully crafted to inspire and transport you to a world of possibilities. Nuru Yako, Your Narrative